Monday, 30 September 2013

Rest In Peace Mack 2B a.k.a Simba [Wateule]


Msanii na producer kutoka kundi la Wateule Malik Ahmed, Mack 2B a.k.a Simba amefariki dunia leo asubuhi huko kwao Yombo. Simba alikuwa akisumbuliwa na kuvimba miguu,hii kwa mujibu wa kaka yake anayejulikana kama Msafiri.Simba ambaye jina lake halisi ni Malick Ahmed alizaliwa Jan 20 mwaka 1980 akiwa mtoto wa mwisho katika familia yao.Wimbo wa 'Ndani ya Party' wa Solo alioshirikishwa Simba ni kati ya ngoma ambazo alionyesha uwezo wake wa kuimba Ragga.Simba ambaye pia alikuwa ni produza mwaka jana alichaguliwa kuwania tuzo za Kilimanjaro kupitia wimbo wake wa 'Paradise'.Kaka wa marehemu amesema atatoa taarifa zaidi za mazishi badae. na kuruhusiwa kurudi nyumbani lakini hali ilibadiliki na leo kufariki. 

Kama ndugu, rafiki na jamaa tunakomba uwajuze wote wasiofahamu...Msiba upo YOMBO MAKARAWE kituo kinaitwa ABIOLA.....M.A.P!!

Rest In Peace Mack 2B Simba 

Sikiliza hapa kwenye sportlights ya power jams [East Africa Radio] akielezea historia yake

No comments:

Post a Comment